SADC kuondoa majeshi yake DRC

JUMUIYA ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika (SADC) imeamua kuondoa vikosi vya majeshi yake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SAMIDRC).

Wakuu wa nchi na serikali SADC walifanya uamuzi huo Machi 13 na wakaelekeza majeshi hayo yaondolewe kwa awamu.

Walifanya uamuzi huo Harare, Zimbabwe kwenye mkutano wa dharura kujadili hali ya usalama nchini DRC ulioongozwa na Mwenyekiti wa SADC, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa.

Advertisement

Rais Samia Suluhu Hassan alihudhuria mkutano huo akiwa katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Katika mkutano huo, wakuu wa nchi na serikali wa jumuiya hiyo ya SADC walipokea taarifa ya hali ya usalama nchini DRC na kuzingatia ripoti ya ujumbe wa kikosi cha SAMIDRC na taarifa ya kamati ya Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC iliyokutana Machi 6, mwaka huu.

Viongozi hao walitoa salamu za pole na rambirambi kwa DRC, Afrika Kusini, Malawi na Tanzania kutokana na vifo vya askari wao wakiwa kwenye kikosi cha SAMIDRC.

Walionesha wasiwasi wao kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama Mashariki mwa DRC, ikiwa ni pamoja na kutekwa kwa miji ya Goma na Bukavu.

Walipongeza askari waliojitolea kusaidia kurejesha hali ya usalama na amani DRC na wakasema kitendo hicho kinaonesha umoja na ustahimilivu.

Viongozi hao walitoa mwito wa kuendeleza ulinzi na kusaidia wananchi wanaotafuta usalama kwa kuzitangia kanuni za kimataifa za utoaji misaada ya kibinadamu lakini pia, wametaka kukomeshwa kwa mashambulizi dhidi ya raia.

Aidha, walitaka mashambulizi hayo pia, yasitishwe na usifanyike uharibifu kwenye miundombinu zikiwemo barabara ili kurahisisha misaada kwa wananchi.

Viongozi hao walibainisha kuwa DRC inahitaji misaada zaidi ya kibinadamu na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa (UN) na Umoja wa Afrika (AU) kusaidia hilo.

Viongozi hao wamekiri linahitajika suluhisho la kisiasa na kidiplomasia kwa pande zote ikijumuisha vyama vya kiserikali, visivyo vya serikali, vya kijeshi na visivyo vya kijeshi katika Mashariki mwa DRC kwa ajili ya kurejesha amani, usalama na utulivu nchini humo.

Pia, wameendelea kusisitiza uamuzi wa mkutano wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na SADC
kuunganisha mchakato wa kutafuta suluhu wa Luanda na Nairobi ili kuimarisha utekelezaji wa jambo hilo.

Walimshukuru Rais wa DRC, Félix Tshisekedi kwa kuendelea kuunga mkono kutatua changamoto za kiusalama zinazolikabili taifa hilo.

Aidha, mkutano huo umempongeza Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia, ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa kuongoza masuala ya amani na usalama ya kikanda SADC.

1 comments
  1. Can you imagine making $18,000 a month while working from home just a few hours a day? I’m doing it, and I never thought it was possible until I found this online opportunity. The work is super easy, and you don’t need any prior experience—just a desire to succeed! I can’t believe how much my life has changed in such a short time. If you’re ready to take control of your income, visit the website and get started today!

    Visit This…… http://www.worksprofit7.com/

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *