Sagini awakilisha wizara maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru
DODOMA: Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini leo Desemba 9, 2023 amewakilisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuungana na Rais Samia Suluhu Hassan kuadhimisha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convertion Centre Jijini Dodoma yameudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kiserikali, Kisiasa, Kidini pamoja na Wananchi huku yakiwa yamebeba kauli mbiu isemayo “Umoja na Mshikamano ni Chachu ya Maendeleo ya Taifa Letu”
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 wenye ujumbe usemao “Ushirikiano Madhubuti wa Kila Mwananchi na Wadau katika Kujenga Tanzania Bora ya Kesho”.
Aidha Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma wameshiriki katika maadhimisho hayo.