Salah kulipwa pauni mil 65 kwa siku Saudia

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah.

TETESI za usajili zinasema mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 32, anatarajiwa kupewa ofa ya malipo ya pauni milioni 65 kwa siku kwa mkataba wa miaka miwili ili kumshawishi aondoke Liverpool kwenda Saudi Arabia majira yajayo ya kiangazi. (Sun)

Mkataba wa Salah katika Klabu ya Liverpool unamalizika Juni 2025 na atakuwa huru kuanza mazungumzo na klabu nyingine kuanzia mwezi huu.

Katika teisisi nyingine Arsenal inafikiria machaguo mbalimbali ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji, huku mshambuliaji wa Sweden anayekipiga Sporting, Viktor Gyokeres, mwenye umri wa miaka 26, na mshambuliaji wa Cameroon uliyeko Brentford, Bryan Mbeumo, mwenye umri wa miaka 25, wakiwa kwenye orodha. (L’Equipe)

Advertisement

Napoli inatarajiwa kujiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 27. (Sun)

Manchester United haitamruhusu Rashford kujiunga na moja ya klabu pinzani za Ligi Kuu ya England, huku Chelsea, Tottenham, na West Ham zikionesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkopo. (Star)