NAMIBIA: SAM Nujoma, kiongozi wa mapinduzi aliyeongoza Namibia kupata uhuru mwaka 1990 na kuhudumu kama rais wa kwanza kwa miaka 15, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.
Anaitwa “baba mwanzilishi” wa Namibia, Nujoma amefariki Jumamosi usiku kufuatia kulazwa hospitalini kwa wiki tatu katika mji mkuu, Windhoek.
Amekuwa wa mwisho kizazi cha viongozi wa Kiafrika walioongoza nchi zao kutoka kwa utawala wa kikoloni au wa wazungu wengine ni pamoja na Nelson Mandela wa Afrika Kusini, Robert Mugabe wa Zimbabwe, Kenneth Kaunda wa Zambia na Samora Machel wa Msumbiji.
Nujoma aliongoza Shirika la Watu wa Afrika Kusini Magharibi (SWAPO) ambalo liliongoza m