Samia atoa mil 583/- ujenzi shule ya Lanchi

SERIKALI ya Samia Suluhu Hassan imetoa fedha Sh milioni 583.5 kufanikisha ujenzi wa shule mpya ya msingi Lanchi iliyopo katika kijiji cha Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 2, 2024. na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dk Pindi Chana mara baada ya uzinduzi wa shule hiyo.

“Ninafurahi kwamba fedha takribani Sh bilioni 42 zimefika kwa wananchi na katika shule hii zaidi ya Sh milioni 500 zimeletwa hapa,” Dk Pindi Chana amesma.
SOMA: Dk Chana akagua chanzo cha maji Miti Mbizi
Amesema Serikali ya Rais Samia ni makini na imeelekeza fedha zifikishwe kwa wananchi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Waziri Chana amewaasa wazazi kuhakikisha watoto wanapelekwa shule kwakuwa urithi wa mtoto ni elimu.

Mkuu wa Shule ya Msingi Lanchi, Augustin Mwambopo amesema mradi huo umesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na umeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Pia amesema umesaidia wanafunzi wanaotoka mbali na eneo la shule na kupunguza matukio ya utoro shuleni.




