RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India.
–
Aidha, kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kupitia ukurasa wa X, Rais Samia ni mwanamke wa kwanza kutunukiwa shahada hiyo hata hivyo ni viongozi wawili tu waliotunukiwa akiwemo Rais wa Urusi, Vladmir Putin na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe.


1 comments