Samia kushiriki mkutano FOCAC
DAR ES SALAAM: Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajia kuhudhuria mkutano wa kilele na wakuu wa nchi na Serikali na jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wenye lengo la kushirikiana katika kuimarisha uchumi utakaofanyika Septemba 4 hadi Septemba 6 nchini China.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema pamoja na mambo mengine mengi mkutano huo utahamasisha viongozi kuongeza kasi ya maendeleo.
SOMA: Rais Samia mwenyeji mkutano wakuu wa nchi Afrika
Aidha amesema katika mkutano huo utakaofunguliwa na Rais wa China Xi Jinping huku wakuu wa nchi nyingine 40 za Afrika watashiriki na wengine kutuma wawakilishi wao na Rais Dk. Samia amepewa heshima ya kutoa huduma akiwakilisha nchi hizo, viongozi wengine watakaoshiriki ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika.
Kupitia Mkutano huo Mikataba ya makubaliano ya masuala mbalimbali yakiwemo ya Uboreshaji wa Reli ya Tazara na uwekezaji mwingine yatasainiwa na Matarajio ni kutengeneza ajira laki mbili zitatengenezwa.
SOMA: Majaliwa amuwakilisha Samia Mkutano SADC