Samia: Mafanikio Tanzania ni maono walionitangulia

RAIS Samia Saluhu amesema mafaniko ya Tanzania yametokana na maono ya viongozi waliomtangulia.

Rais Samia amesema hayo leo katika maadhimisho ya sherehe za miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa kwanza wa itaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete.

Amewataja viongozi hao kuwa Hayati Mwalimu Nyerere, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Hayati Benjamini Mkapa, Rais mstaafu Jakaya Kikwete na Hayati John Magufuli.

Advertisement

Amesema kwa maono makubwa ya viongozi hao ndio wamefanikisha taifa kupiga hatua katika sekta mbalimbali.

Rais Samia ameahidi kuendelea mema yote, kujifunza kutokana na changamoto walizokutana nazo viongozi hao.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *