Samia: Tuiombee nchi idumu katika amani, umoja

DAR ES SALAAM; RAIS Samia Suluhu Hassani, amewaomba Watanzania waungane kuiombea nchi iendelee kudumu katika amani, umoja na utulivu.

Rais Samia ameandika katika mtandao wake wa kijamii wa X: Nawatakia nyote kheri katika Sikukuu ya Krismasi. Tusherehekee na kujumuika na familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa furaha na upendo.

“Historia ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo itupe pia tafakari juu ya mwanzo mpya katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku, juu ya upendo kwa ndugu na jirani, juu ya uzalendo kwa Taifa letu, juu ya kuishi katika kweli, juu ya unyenyekevu tunapojaaliwa nafasi za kuwatumikia wenzetu, na juu ya shukrani.

Advertisement

“Tuungane pia kuiombea nchi yetu iendelee kudumu katika amani, umoja na utulivu. Mwenyezi Mungu awabariki nyote”.