Sanaa, burudani zaongoza kwa ukuaji

DODOMA; SEKTA ya sanaa na burudani ni miongoni mwa sekta tano zilizoongoza kwa ukuaji mwaka 2024.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2024 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2025/26.
“Katika mwaka 2024, sekta tano ziliongoza kwa ukuaji ni sanaa na burudani (17.1%), uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme (14.4%), habari na mawasiliano (14.3%), fedha 8 na bima (13.8%) na afya (10.1%).
“ Sekta tatu zilichangia takribani nusu ya pato la taifa. Sekta hizi ni kilimo (26.3%), ujenzi (12.8%) na uchimbaji wa madini na mawe (10.1%). Tunachohitaji kwa siku za usoni ni kuongeza tija zaidi kwenye uzalishaji ili kilimo kiwainue Watanzania wengi zaidi kimapato,” amesema Prof. Mkumbo.