SANAMU ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere imezunduliwa katika Bustani ya Mashujaa iliyopo mji mkuu wa Kuba, Havana.
Uzindizi huo umefanywa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro pamoja na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kuba, Anayansi Rodriguez Camejo.
SOMA: Taasisi yaenzi miaka 101 ya Nyerere
Uzinduzi huo pia umeshuhudiwa na Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania na Kuba, Makatibu Wakuu na Maafisa wengine Waandamizi kutoka pande zote mbili.
Kuzinduliwa kwa sanamu hiyo ni jitihada za Serikali ya Kuba na Tanzania katika kuenzi mchango wa Hayati Nyerere katika kuimarisha ushirikiano wa mataifa hayo mawili.