Saratani yaendelea kuwa tishio

TAKWIMU za mwaka 2022 zinaonyesha kuna ongezeko la wagonjwa wapya wa saratani 45,000 hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitengo cha saratani kwenye Hospitali ya Shifaa Pan African jijini Dar es salaam Waziri wa Afya Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kuunga mkono wawekezaji binafsi kwenye sekta ya afya ili kukabiliana na ugonjwa huo.

Waziri Jenista amesema saratani tano zinazoongoza hapa nchini ni kizazi asilimia 24.2, tezi dumi asilimia 10.7, matiti asilimia 10, koo asilimia 7.9 na utumbo mpana asilimia 4.9.

Advertisement

SOMA: ‘Saratani yaua 27,000 kila mwaka nchini’

Aidha amesema katika asilimia 44.2 ya wagonjwa wote saratani za mlango wa kizazi na matiti ndizo zinaadhiri zaidi wanawake.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Shifaa pan African, Bashir Haroon amesema mradi huo wa huduma za kutibu saratani una uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 60 katika kuisaidia serikali kwenye sekta ya afya ili wananchi wapate tiba stahiki.

Amesema taasisi hiyo ipo katika kuunga jitihada za serikali na kuwapa motisha madaktari wa kitanzania katika sekta hiyo ya afya.