Sekondari yapongezwa upandaji miti

MTWARA: SHULE ya Sekondari Shangani iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani imetajwa ni miongoni mwa vinara katika suala la utunzaji wa mazingira na upandaji miti ya mbao na matunda.

Kaimu Mhifadhi Wilaya ya Mtwara, Ashraf Hussein amesema hayo baada ya kulitembelea shule hiyo ili kuona shughili za uendelezaji upandaji miti pamoja na utunzaji wa mazingira.

Ashraf amesema taasisi za shule zimehamasika katika suala la upandaji miti  na kumekuwepo na shule za mfano wa upandaji miti ambapo ushahidi wa matokeo yake yameonekana ikiwemo Shule ya Sekondari Shangani.

“ Shule hii inawezekana ni darasa huru kwa baadhi ya shule kwenda kujifunza jinsi ya uhifadhi wa miti waliyoipanda na miti hii  imefanya iwe ni moja wapo ya kutumika  kama eneo la stadi za mafunzo kwa wanafunzi wetu wanaosoma katika shule mbalimbali za sekondari,”amesema Ashraf.

Ashraf amesema wakala utaendelea kutoa hamasa kwa shule nyingine za Sekondari ambayo nyingine zimegawiwa miche ya miti na matokeo yake ni mazuri.

“Tunazihimiza shule ambazo hazijapanda miti zije kujifunza katika Shule ya Shangani ili kuona uhufadhi ulivyofanyika kwa miti kuota vizuri na kupata madhari mazuri ya Shule na wanafunzi kuendelea kupata elimu kwa uhalisia kwa macho kuhusiana na utunzaji wa miti na umuhimu wa miti inayopadwa,”amesema Ashraf.

Naye, mwalimu wa shule hiyo, Paul Ndomba amesema shule hiyo imekuwa ni kinara kwenye upandaji miti  kutokana na  kuwepo wa  ushirikiano na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Kanda ya Kusini.

Mwalimu huyo ambaye ni mdau wa mazingira amesema shule imepanda miti ya mbao ‘mitiki’ na mingine zaidi ya 4,000.

Kwa miti ya matunda katika msimu wa mwaka huu (2026)imepandwa miti 600 na zoezi linaendelea  katika kipindi hiki cha mvua.

Amesema miti iliyopandwa imekuwa na faida kubwa shulen hapo hasa kipindi cha kiangazi chenye jua kali na madarasani uwezi kufanyia kazi, hivyo wanatumia vivuli vya miti hiyo  wao na wanafunzi kukaa na kuendelea kujifunza .

Ndomba alisema pia wanatumia kuwepo kwa miti hiyo kuwafundisha wanafunzi kwa vitendo kuanzia mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne.

Pia amesema shule imeweka utaratibu wa kila mwanafunzi wa kidato cha kwanza anapofika shuleni anakabidhiwa mti wake aupande.

“Anapomaliza miaka minne miongoni mwa vitu atakavyokabidhi ni pamoja na mti alioupanda na endapo ukikauka anaupanda mwingine,”amesema Ndomba.

Ndomba amesema mpango huo unaenda vizuri, moja ya changamoto ambayo  anaiomba Serikali, TFS na wadau wengine ni kutekeleza agizo ya serikali ya upandaji miti milioni moja kila mwaka hasa kwa halmashauri nchini.

Wanafunzi wa shule hiyo, Janeth Unga anayesoma kidato cha tatu amesema miti iliyopandwa shuleni inawasaidia kupata kivuli wakati wa joto kali wanatoka darasani na kusomea kivulini au muda wa chakula cha mchana.

“ Miti hii pia inatumika na kujifunza kwa vitendo somo la baolojia kwa wanafunzi wa kidato cha nne na pia faida nyingine ni kutunda mazingira na kuzuia mmomonyoko wa udongo maeneo haya ya shule” amesema  Unga.

Mwanafunzi mwengine wa Kidato cha nne ,Jackson Sanyiwa amewahimiza   wanafunzi na wananchi wa wilaya ya Mtwara wajenge tabia ya kupanda miti kwa wingi kwani inafaida nyingi  ikiwemo  kukabiliana na mabadiliko ya tabiaanchi,  kupata mbao, matunda na hewa safi .

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..  https://www.payathome9.place

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

    2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
      .
      This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do…..

     https://www.payathome9.place

  3. Google paid $200 a hour on the internet..my close relative has been without labor for nine months and the earlier month her compensation check was $51005 by working at home for 10 hours a day….. E­v­e­r­y­b­o­d­y m­u­s­t t­r­y t­h­i­s j­o­b n­o­w b­y j­u­s­t u­s­e ­t­h­i­s

    GOOD LUCK.:) http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button