Serikali: Daktari aliyefeli asiendelee na mafunzo

DODOMA; Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameliagiza Baraza la Madaktari nchini, lisiruhusu daktari aliyefeli mtihani wa utarajali kuendelea na mafunzo kwa vitendo, badala yake itamlazimu arudie mtihani huo mpaka afaulu ndipo aendelee na mafunzo kwa vitendo (Internship).

Aidha Ummy amelitaka baraza hilo kuzingatia miongozo ya alama za ufaulu kama ilivyoelekezwa, ili kusimamia taaluma ya udaktari na endapo daktari atashindwa kufikia alama zilizopendekezwa kwenye muongozo itabidi arudie mitihani.

Akizumgumza leo jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa kamati huru kuhusu ufaulu wa mitihani ya watarajali inayoendeshwa na baraza  hilo,  amesema daktari yeyote aliyemaliza masomo yake katika vyuo vya udaktari ndani na nje ya nchi, ili apate leseni ya udaktari ni lazima afanye mtihani wa kabla ya utarajali na baada ya kukamilisha kipindi cha utarajali.

Pia ummy ameliagiza baraza hilo kuendelea kuendesha mitihani miwili ya kabla na baada ya utarajali kwa madaktari wote nchini, wanaomaliza vyuo na kuanza mafunzo kwa vitendo.

Amesema wataendelea kutimiza jukumu la kumlinda mwananchi kwa kuhakikisha anapata huduma bora kutoka kwa wanataaluma wa afya waliothibitishwa na Mabaraza ya kitaaluma kuwa ulinganifu na ubora unaotakiwa utakaowezesha kutoa huduma za afya bora kwa wananchi.

Akiwasilisha mapendekezo ya kamati, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof. Mohammed Kambi, amesema kamati imependekeza mitihani ya utarajali kuendelea kufanyika licha ya madaktari kulalamikia ufaulu mdogo, huku akilitaka baraza  hilo kutoa alama za ufaulu kwa madaktari waliofanya mitihani hiyo.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
1 month ago

Cash generating easy and fast method to work in part time and earn extra $15,000 or even more than this online. By working in my spare time i made $17,000 in my previous month and i am very happy now because of this job.
.
.
Detail Here——————————————————–>>>  http://Www.BizWork1.Com

BarbaraBirch
BarbaraBirch
1 month ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by BarbaraBirch
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x