‘Serikali imejizatiti matengenezo miundombinu ya umeme’

Miundombinu ya Umeme

SERIKALI imeongeza bajeti ya matengenezo ya miundombinu ya umeme kutoka Sh bilioni 197.61 kwa mwaka 2021/22 hadi Sh bilioni 211.56 kwa mwaka 2022/23 ili kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini.

Hayo yalielezwa bungeni, jijini Dodoma wakati Waziri wa Nishati, January Makamba alipowasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, utekelezaji wa maazimio ya Bunge kutokana na taarifa ya mwaka ya k

Kamati hiyo imeelezwa kuwa, ongezeko hilo la bajeti limefanywa ili kuhakikisha matengenezo ya miundombinu yanafanyika kikamilifu na kwa wakati na hivyo kuimarisha hali ya upatikanaji umeme.

Advertisement

Pamoja na hilo, January alisema serikali imetenga Sh bilioni 500 kwa ajili ya mradi wa kuimarisha gridi ya Taifa ambao unalenga kuboresha hali ya umeme nchini.

Pamoja na kazi nyingine, alisema kilometa 3,930 za njia ya usafirishaji umeme zitajengwa, vituo vikubwa vya umeme 62 vitajengwa na kilometa 2,572 za njia za usambazaji umeme zitajengwa pia.

Kuhusu utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), January alisema mradi huo ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 67.18, unaendelea kutekelezwa kwa ufanisi kwani kuna vitengo kutoka Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vinavyosimamia mradi huo na pia kuna kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara wanaosimamia mradi.

Aidha, alisema ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji umeme wa kV 400 kutoka JNHPP hadi Chalinze ambapo kunajengwa pia kituo cha kupoza umeme, umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika Januari mwakani, hali itakayowezesha umeme kutoka mradi huo kutokumbwa na changamoto ya usafirishaji na usambazaji.

Kuhusu suala la ujenzi wa maghala makubwa ambayo yatahifadhi mafuta zaidi ya mita za ujazo milioni 1.25 na kuiwezesha nchi kuagiza mafuta mengi zaidi wakati bei ya mafuta inaposhuka katika soko la dunia, alisema Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea na mkakati huo.

Lengo alisema ni kuhifadhi mafuta yatakayotumika pia kama hifadhi ya Taifa ya mafuta ya kimkakati.

 

 

/* */