WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema serikali inakusuia kuanzisha Wakala wa Ugani utakaowasimamia maofisa wa ugani nchini ili kada hiyo iweze kuheshimika na itambulike kama zilivyo kada nyingine.
Lengo ni kuleta ufanisi kwenye sekta ya kilimo na kuhakikisha kunakuwa na usalama wa chakula nchini.
Waziri Bashe amesema hayo katika hotuba yake wakati wa hafla yakutoa zawadi kwa wanafunzi na wahadhiri waliofanya vizuri kwa mwaka 2023 / 2024 pamoja na wadau wengine waliosoma na kufanya kazi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Bashe amesema serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika kuona sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi , malisaili na zingine zinazoleta matokeo mazuri katika uzalishaji ili kukuza uchumi.
Kwa kutambua hilo kwenye sekta ya kilimo amesema kwake ofisa ugani ni sawa na daktari na kwa umuhimu wao ,serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha Wakala wa Ugani .
Bashe amesema wakala huo utatungiwa sheria, kanuni na taratibu ili kuwatambua maofisa ugani kuwa ni taaluma kama ilivyo kwa kada nyingine zikiwemo za uhasibu .
“ Lengo ni kuifanya kada hii iheshimike na itambulike kwani bila kuwa na maofisa ugani wanaotambulika kisheria huwezi kuwa na uhakika wa usalama wa chakula nchini,” amesema Bashe.
SOMA: Bashe awatoa wasiwasi wakulima wa mahindi
Waziri Bashe amesema licha ya kusudio hilo, serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi na rafiki ya kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika sekta ya kilimo kupitia programu ya BBT.
Amesema program hiyo imeonesha ushiriki ni mkubwa kwa watoto wakike kwani vijana 200 walioajiriwa kutokea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA),uwajibikaji kwa watoto wakike ni vizuri zaidi kuliko wanaume.
“ Watoto wakike wanaishi vijijini na wakulima na mafanikio haya ndiyo yaliyonusukuma mimi Waziri kwanda kwa Mheshimiwa Rais kuomba kuajiri vijana wengine 200,” amesema Bashe.
Waziri Bashe amesema katika matokeo yaliyopatikana kwenye vijiji 50 kupitia program ya BBTni makubwa zaidi na pia kupitia program hiyo chini ya vijana hao imewezesha kubaini wakulima hewa waliopatiwa pembejeo za kilimo.
“ Katika vijiji hivyo walivyopelekwa vijana hawa tuliwapa taarifa ya wakulima waliosambaziwa pembejeo (Mbegu) na walipowafuatilia tuliletewa wakulima hewa zaidi ya asilimia 60,” amesema Bashe
Waziri Bashe amesema kutokana na ripoti hiyo wizara yake kwa mwaka huu inakwenda kufuta utaratibu unaotumika na kuweka mpya utakaokuwa na usimamizi wa Vijana hayo waliopelekwa vijijini.