Serikali yaahidi suluhisho kupanda mafuta

KUPANDA kwa bei ya mafuta nchini kumesababisha ongezeko la nauli za usafiri mkoani Kilimanjaro, hali ilivyowaathiri abiria na watoa huduma za usafiri. Baadhi ya madereva wa vyombo vya usafiri, wakiwemo wa bodaboda na bajaji, wameiomba Serikali kuingilia kati na kupunguza bei ya mafuta ili kuwezesha shughuli za usafiri kuendelea kwa ufanisi.
Dailynews Digital ilizungumza na mmoja wa madereva wa bodaboda Abuu Abubakar Shabani amesema wamelazimika kupandisha nauli ili kukabiliana na gharama za mafuta hatua ambayo ambayo imepunguza idadi ya abiria. “Tumepandisha nauli lakini abiria wamepungua kwa sababu wengi wanasema hali ya uchumi ni ngumu,” amesema. SOMA: Serikali yaeleza hali ya upatikanaji mafuta
Kwa upande wake dereva bajaji Hoza Omary amesema ingawa wanaongeza nauli ili kupata faida, wananchi wa kipato cha chini ndio wanaoumia zaidi, hivyo kuiomba Serikali kutafuta suluhisho. Nao abiria wameeleza kuathirika na ongezeko hilo la kupanda kwa mafuta ambapo nauli zimepanda na kuwalazimu kubadili bajeti yao ya kila siku. “Nilikuwa natumia shilingi 2,000 kwa siku kwa nauli, lakini sasa natumia kiasi hicho kwa safari moja tu,” alisema Hermina Kimaro.
Hatahivyo, wameongezea kuwa hali ya uchumi mkoani humo bado ni tete kufuatia mafuriko ya hivi karibuni hivyo kupanda kwa bei ya mafuta kunazidi kuongeza ugumu wa maisha. Kwa ujumla, wadau hao wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kupunguza bei ya mafuta ili kupunguza mzigo kwa wananchi.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity……….
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com