Serikali yakabidhi vifaa vya mafunzo vyuo 63

KATIBU Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amekabidhi vifaa vya mafunzo vyenye thamani ya Sh Bilioni 8.4 kwa vyuo 63 vya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).
SOMA: Vyuo vya ufundi viwekeze katika vifaa vya kufundishia
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2025 jijini Dar es Salaam, katika Mkutano wa VETA na Wamiliki wa Viwanda, Waajiri na Wadau wa mafunzo ya Ufundi Stadi.
Vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kuboresha mazingira kufundisha na kujifunza kwa vitendo.
Vifaa hivyo vimenunuliwa na Serikali kwa fedha zilizotengwa katika bajeti ya Mwaka wa fedha 2024/25 kwa lengo la kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi nchini.



