Serikali yaleta mageuzi Z’bar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hus sein Mwinyi amesema serikali imeleta mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kutokana na Mapinduzi ya Mwaka 1964.

Sambamba na hilo, Dk Mwinyi amewataka wana siasa na viongozi wa dini kutunza na kuenzi amani katika mahubiri yao hususani kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu ili kuifanya Zan zibar kuwa na manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Rais Dk Mwinyi alisema hayo jana wakati akihutubia wananchi kwenye kilele cha Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika Janu ari 12, 1964. Alisema Mapinduzi ya Zanzibar yameleta mafanikio kiuchumi kwa kufanikisha ongezeko katika ukusanyaji wa mapato pamoja na kud hibiti matumizi yake.

Advertisement

Aidha, Dk Mwinyi alion geza kuwa Mapinduzi ya Zanzibar yamewezesha wa nanchi kiuchumi pamoja na kuimarisha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege, bandari, ujenzi wa nyumba za makazi na biashara.

“Mapinduzi yametuwezesha kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano wa watu wa Zanzibar na wanaishi kwa usawa. Tunafurahia mafanikio yaliyopatikana na mapinduzi,” alisema Dk Mwinyi.

Alisema serikali imefanikiwa kuimarisha demokrasia na utawala bora na kuwapongeza Wazanzibari wote kwa mafanikio hayo.

Aliwakumbusha wananchi kuwa mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu hivyo wanatakiwa kujitokeza kush iriki uchaguzi huo kwa amani na utulivu akiongeza kuwa wananchi wote washiriki kwa amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

“Tayari tume zetu za uchaguzi za INEC na ZEC zimeanza kuchukua hatua za matayarisho ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa misingi ya haki na ya kishe ria, hivyo tuendelee kutoa ushirikiano kwa tume zetu ili ziweze kufanikisha hilo,” aliongeza Dk Mwinyi.

Alitoa wito kwa wana siasa, taasisi za kijamii na viongozi wa dini na wananchi wote kuendelea kudumisha amani, utulivu na umoja wa kitaifa ili taifa lizidi kupiga hatua za maendeleo kwa faida ya waliopo na vizazi vijavyo.

“Tuendelee kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, umahiri na uzalendo kwa kuweka mbele maslahi ya nchi yetu kama walivyofanya waasisi wa taifa hili,” alisema. Katika hotuba yake ya Miaka 61 ya Mapinduzi aliyoitoa juzi, Rais Mwinyi alisema dhamira ya Mapinduzi inaendelea kutimizwa kwani uchumi wa Zanzibar umeendelea kuimarika na hadi kufikia Septemba 2024, ulifika asilimia 7.5.

Dk Mwinyi alisema pato la taifa kwa bei ya soko (GDP) limeongezeka kufikia thamani ya Sh trilioni 6.04 mwaka 2023 kutoka Sh trilioni 4.78 mwaka 2021 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 26.

Aidha, alisema sekta ndogo ya huduma za watalii imeimarika kwani idadi ya watalii wanaotembelea Zanzi bar imeongezeka kwa asilimia 145 katika kipindi hicho.

Alibainisha kuwa ukusanyaji wa mapato ya serikali umeongezeka kwa asilimia 51 kutoka Sh bilioni 858.2 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Sh trilioni 1.3 mwaka 2022/2023.