Serikali yanunua mtambo wa Sh bil 2.9 Maabara ya Mkemia Mkuu
DAR ES SALAAM: MKURUGENZI wa Huduma za Sayansi Jinai, David Elias amesema serikali imefanya uwekezaji mkubwa, wa kisasa ikihusisha manunuzi ya mtambo mkubwa uliogharimu Sh bilioni 2.9 kwaajili ya kutumika katika Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchakata sampuli mbalimbali.
Mtambo huo unachukua sampuli zaidi ya 200 kwa muda mmoja na matokeo kupatikana haraka muda usiozidi saa moja, lengo ni kurahisisha huduma kwa kwa wawekezaji na wafanyabiashara.
SOMA: Mkemia: Hakuna dereva anayepoteza maisha kwa kemikali
Amesema hayo leo, Julai 11, 2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2024) katika viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Elias amesema Sifa za mtambo huo ni pamoja na kupeleka sampuli mbalimbali na kuweza kufanya kazi saa 24 na matokeo yake ya uchakataji wa sampuli kutoka kwa wakati
Pia, Mkurugenzi huyo amesema mtambo huo kwa sasa unapatikana makao makuu Dodoma lengo la kuweka huduma hiyo kati kati ya Nchi ni kuwawezesha watu wote kuweza kupata huduma hiyo
Uwekezeji uliofanyika wa mitambo ya kisasa mikubwa ni kwaajili ya wananchi ili waweze kufanya biashara vizuri na ili waweze kuwekeza vizuri
“Hii ni mitambo ambayo imenunuliwa na serikali kwaajili ya wananchi wake ili waweze kufanya biashara vizuri na ili waweze kuwekeza vizuri” amesema David Elias