Serikali yaongeza uwezo wa kuhifadhi  chakula

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema  tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe imebaini kuwa na upungufu wa uzalishaji katika  baadhi ya maeneo katika msimu wa 2021/2022 uliotokana na  athari za mabadiliko ya tabianchi, hali iliyosababisha kupanda  bei kwa baadhi ya mazao ya chakula.

Ameyasema hayo leo Mei 8,2023 akiwasilisha bajeti ya Wizara ya Kilimo bungeni mjini Dodoma na kwamba ili kukabiliana na hali hiyo, wizara kupitia NFRA ilichukua hatua za kusambaza chakula.

“Wastani wa tani 75,282.30 za mahindi na kuuzwa kwa bei ya chini  ya soko kati ya Shilingi 680 hadi 920 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya soko ya Shilingi 1,200 hadi 1,500 lengo likiwa ni kumlinda  mlaji na kudhibiti mfumuko wa bei,” amesema Bashe.

Amesema,  ili kukabiliana na upungufu wa chakula, Serikali inaendelea kuongeza uwezo wake wa kuhifadhi chakula kutoka tani 251,000 za sasa hadi tani 506,000.

Aidha, kwa sasa Serikali imeanza shughuli ya upembuzi yakinifu kwa ajili  ya kujenga miundombinu ya uhifadhi itakayoongeza uwezo wa kuhifadhi kufikia tani 3,000,000 ifikapo mwaka 2030.

” Lengo ni kuhakikisha kuwa, Taifa letu lina uwezo wa kuhifadhi chakula cha kutumia miezi sita pindi inapotokea janga ili kulinda uchumi wetu, heshima yetu, utu wetu na uhuru wetu,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x