WACHAMBUZI wa siasa na diplomasia wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuimairisha uhusiano na mataifa mengine na kuiwezesha nchi kuimarisha uchumi.
Mchambuzi wa masuala ya uchumi, Profesa Haji Semboja amesema uhusiano wa taifa moja na lingine unajengwa kwa sera, sheria nzuri na wepesi wa kiongozi wa nchi kutembelea wenzake katika nchi zao.
Profesa Semboja amelieleza gazeti la HabariLEO kuwa Rais Samia anaaminiwa na anashirikishwa kwenye masuala ya amani na inakuwa hivyo kwa sababu anaisimamia vizuri nchi yake.
“Rais Samia amefanya vizuri kwenye mifumo ya taasisi na mahusiano mazuri na mataifa mengine, amekuwa mwepesi kama kiongozi kuhakikisha katika kila kitu tulichokubaliana kama taifa tunashirikiana na mwenzatu,” alisema Profesa Semboja.
Aliongeza: “Tumeona na wenzake wanakuja nchini, kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali tumeona uwekezaji umeongezeka katika uongozi wake, tukisema mtu kijamii yupo vizuri tunaangalia kama una mahusiano mzuri na majirani zako na kama wanakuja kwako na wewe kwenda kwa wengine, huo ndio uhusiano mzuri wa jamii”.
Mchambuzi wa masuala ya diplomasia, Goodluck Ng’ingo alisema ziara za Rais Samia nje ya nchi zimeimarisha sekta binafsi na shughuli za kibiashara.
“Ukuaji wa kiuchumi, utekelezaji wa ile falsafa yake ya diplomasia ya uchumi hiyo imeweza kufanywa kwa kiasi kikubwa na ndio maana tumeweza kuwa na mikutano ya taasisi mbalimbali, shirikisho la mambo ya kilimo mwaka jana na sasa hivi mambo ya nishati na mengine kadha wa kadha,” alisema Ng’ingo.
Alisema uhusiano mzuri wa kidiplomasia wa Tanzania na mataifa mengine umesaidia kuimarisha ulinzi kwenye mipaka.
“Unaweza kuona vitendo vya uhalifu mipakani vimepungua, mathalani Mtwara watu wote wa vikundi vile vya kigaidi wamepotea kutokana na ushirikiano ulipo kati yetu na Msumbiji,” alisema.
Ng’ingo alisema pia Serikali ya Awamu ya Sita imeboresha miundombinu yakiwemo madaraja, reli na mabwawa ya umeme mambo ambayo ni muhimu katika ujenzi wa uchumi na akatoa wito kwa sekta binafsi zitumie fursa ili uchumi usimilikiwe na wageni.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini amempongeza Rais Samia kwa kurudisha uhusiano wa kidiplomasia na kuiunganisha nchi na mataifa mengine.
“Kuwa na mahusiano na nchi na mashirika ya nje kuna faida kiuchumi, kuna kukutana na wafanyabiashara na wawekezaji na kuunganisha watu wa Tanzania na watu wa nje,” alisema Selasini.
Amewapinga wanaombeza Samia wakidai anazungukazunguka na akasema safari za Rais nje ya nchi zinaitangaza Tanzania.
Mchambuzi wa siasa za kimataifa, Aloyce Mchunga alisema katika miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita nchi imefunguka na uchumi wa nchi unaimarika.
Mchambuzi wa masuala ya diplomasia na siasa, Abdulkarim Atiki amesema Rais Samia ameibadilisha nchi kidiplomasia.
“Katika miaka minne ya uongozi wake amepata mafanikio makubwa, uwekezaji wa nje umekuwa mkubwa zaidi na
inaleta faraja sana katika ukuaji wa uchumi,” alisema Atiki.
Mchambuzi wa siasa na diplomasia, Abdallah Kanju alisema Rais Samia ameongeza ushirikiano na mataifa mengine katika uchumi kwa kukaribisha kampuni kuwekeza nchini.
“Mfano mzuri kwa hapa nchini amemkaribisha DP World kuwekeza katika Bandari ya Dar es Salaam na matokeo chanya yameonekana,” alisema Kanju.
Kanju alisema Rais Samia ameongeza ushirikiano wa kikanda kwa upande wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa kuwa mstari wa mbele kutatua migogoro.
Imeandikwa na Eva Sindika na Prisca Pances.
I seriously love your blog.. Very nice colors & theme.
Did you develop this web site yourself? Please reply back
as I’m attempting to create my own site and would like to know where
you got this from or what the theme is called. Cheers! https://blog-kr.Dreamhanks.com/question/gateaux-personnalises-creativite-et-delice-a-chaque-occasion-166/
Can you imagine making $18,000 a month while working from home just a few hours a day? I’m doing it, and I never thought it was possible until I found this online opportunity. The work is super easy, and you don’t need any prior experience—just a desire to succeed! I can’t believe how much my life has changed in such a short time. If you’re ready to take control of your income, visit the website and get started today!
Visit This…… Www.EarnApp1.Com