Serikali yatahadharisha mtumizi holela ya antibiotiki

SERIKALI imetahadharisha matumizi mabaya ya dawa za antibiotiki ambazo zinasababisha usugu wa vimelea dhidi ya dawa, ikionya hatari ya kutokea madhara makubwa hasa kifo kwa watumiaji.

Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema jijini Dar es Salaam kuwa takwimu zinaonesha asilimia 92 ya antibiotiki zinatumika nchini  zimesababisha usugu kwa asilimia 59.8.

Amesema eneo lililoathrika zaidi ni la uvuvi na ufugaji ambapo asilimia 90 ya dawa hizo hutumika kutibu wanyama badala ya chanjo.

“Tumetengeneza mpango kazi mpya wa kitaifa kupambana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa,” amesema Profesa Nagu. “Tunategemea kupokea taarifa ya utekelezaji ya mpango kazi wa taifa wa mwaka 2017-2022.”

Tanzania inakabiliwa na usugu wa vimelea dhidi ya dawa, tatizo ambalo limeendelea kushamiri katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara.

 

Habari Zifananazo

Back to top button