Serikali yazungumzia upatikanaji fedha za kigeni

Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba.

SERIKALI imesema pamoja na changamoto zilizojitokeza hali ya upatikanaji wa fedha za kigeni nchini imeendelea kuwa himilivu.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Septemba 8, 2023 na Waziri wa Fedha, Dk.

Mwigulu Nchemba alipokuwa akibu swali la Mbunge wa Biharamulo Magharibi, Injinia Ezra Chiwelesa, aliyetaka kujua mpango mpango wa serikali katika kunusuru uchumi wa nchi kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni, hususani dola ya Kimarekani.

Advertisement

Akijibu swahilo hilo Waziri Nchemba amesema serikali inaendeleea kuchukua hatua mbalimbali za muda mfupi, wa kati na muda mrefu katika kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa fedha za kigeni,hususani dola ya Marekaninchini.

“Changamoto hiyo imesababishwa na athari za mgogoro wa vita kati ya Ukraine na Urusi, kuimarika kwa shughuli za kiuchumi na kijamii baada ya UVIKO-19 na mabadiliko ya tabianchi.

“Sababu nyingine ni utekelezaji wa sera za fedha ambayo inalenga kupunguza ukwasi katika uchumi wa nchi mbalimbali ikiwemo Marekani ili kukabiliana na ongezeko la mfumuko wa bei.

“Kwa ujumla matukio hayo yameathiri mnyororo wa uzalalishaji, usambazaji na uhitaji wa bidhaa na huduma katika soko la dunia,” amesema na kuongeza kuwa:

“Pamoja na changamoto zilizojitokeza hali ya upatikanaji wa fedha za kigeni nchini imeendelea kuwa himilivu ambapo akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani milioni 5,246.7 mwezi Julai 2023, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4.7 ikilinganishwa na malengo ya miezi mine,” amesema.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *