Serikali Zanzibar kushirikisha sekta binafsi huduma za hospitali

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ya Zanzibar imekuja na utaratibu mpya wa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma kwa hospitali za serikali ikiwemo maabara, utoaji wa dawa, huduma za Xray na Ultra sound, chakula pamoja na usafi lengo ni kutoa huduma bora za kisasa na za haraka kwa Wananchi.
Kiongozi huyo amesema hayo leo wakati akifungua Hospitali ya Wilaya ya Kivunge, Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kuelekea shamra shamra za miaka mitatu ya Serikali ya awamu ya nane madarakani katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Oktoba 23, 2023.
Aidha Dk Mwinyi amefungua Hospitali ya Kivunge na baadaye kuweka Jiwe la Msingi katika ujenzi unaoendelea wa skuli ya ghorofa Donge Mkoa wa Kaskazini Unguja leo tarehe 23 Oktoba ,2023.
Vilevile Dk Mwinyi amewahakikishia Wananchi serikali itaendelea kujenga skuli za msingi na sekondari za ghorofa kwa pesa ya serikali, ujenzi wa barabara, miradi ya maji na miradi ya maendeleo yote kwa pesa za Serikali.
Amesema wapigaji makelele wachache ni wale wabadhirifu na mafisadi ambao mirija yao imezibwa kwa sasa Serikali malengo yake fedha zinakwenda kwenye miradi ya huduma za kijamii, mishahara ya wafanyakazi wa serikali, pensheni kwa wastaafu na jamii.
4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *