Sh milioni 200 zatengwa majukwaa ya wanawake

KWA mwaka 2023/24, Serikali imetenga Sh milioni 200 kwa ajili ya kugharamia majukwa ya wananake.

Haya yameelezwa jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Exaud Kigahe wakati wa kujibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Subira Mgalu (CCM).

Katika swali lake la msingi, Mgalu alitaka kujua ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya uendeshaji wa Mabaraza ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi.

Akijibu swali hilo, Kigahe alisema Serikali imekuwa ikiendesha Majukwaa (siyo Mabaraza) ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi tangu mwaka 2017.

Amesema lengo kuu la Majukwaa hayo ni kuwakutanisha wanawake ili waweze kujadili fursa za kiuchumi na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi nchini.

Amesema hadi kufikia mwaka 2021/2022, Mikoa yote 26 imezindua Majukwaa ya wanawake, Halmashauri 140 kati ya Halmashauri 184, Kata 1,149, kati ya Kata 2,404, Mitaa/Vijiji 1,776, kati ya Mitaa/ vijiji 7,613.

Kigahe amesema katika kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga zaidi ya Sh milioni 72 na kwa mwaka 2023/ 2024 imetenga Sh milioni 200 kwa ajili ya uendeshaji wa majukwaa hayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button