Sh milioni 27 kukuza uchumi wananchi Madumba

WANANCHI katika kijiji cha Madumba Halmashauri ya Mji wa Newala mkoani Mtwara watanufaika kiuchumi baada ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuvipatia vikundi saba vyenye walengwa 86 jumla ya Sh milioni 27.2 kwa ajili ya kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya.

Mkurugenzi wa mradi wa Tasaf, John Stephen kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo amesema halmashauri hiyo ina jumla ya vikundi 243 ambavyo vimepatiwa zaidi ya Sh milioni 400 ikiwemo vikundi hviyo saba.

Advertisement

Mkoa huo una vikundi mbalimbali vya kuweka akiba na kukuza uchumi wa kaya ndani ya kaya za walengwa 4,000 kati ya hivyo vikundi 243 viko kwenye halmashauri hiyo.

Lengo la ziara hiyo katika halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi huo ambayo hufanyika kila baada ya miezi sita ili kujionea hatua mbalimbali walizofikia katika utekelezaji wa mradi ikiwemo mfanikio, changamoto ili kama zipo waangalie namna ya kuzitatua.

‘’Mpaka sasa tunaekelekea kumaliza ziara lakini tumepata mafanikio makubwa sana katika hii ziara kwa kuona kwamba vijiji tulivyovitembelea madumba, msilili vinatekeleza mradi wa Tasaf vizuri sana tumeona kila eneo ambalo Tasaf na wafadhili wake wanasaidia katika hivi vijiji mambo yamekwenda vizuri sana’’, amesema Stephen

Hata hivyo kukusanya maoni ya wadau mbalimbali kutoka katika ngazi tofauti tofauti kama vile mkoa, wilaya, kata mpaka kijiji ili waone namna ambavyo wanaweza kuboresha mradi huo.