Sh millioni 200 kujenga zahanati Mirerani

SERIKALI imetoa Sh milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati mgodini Mirerani

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema hayo kwa njia ya simu katika mkutano wa Katibu wa Hapmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa(CCM-NEC), Amos Makalla akiwa anazungumza na wananchi Wilaya ya Simanjiro Manyara.

SOMA: Hospitali mpya 135 za wilaya zajengwa 

Awali Mchengerwa alisema kuwa dhamira yao kama wizara ni dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan na lengo lao ni kuona watanzania wanapata huduma bora za afya zikiwa karibu na maeneo yao ya makazi.

Aliongeza kuwa mkurugenzi ameshaanza utaratibu kwa kushirikiana na wadau na wa OR-Tamisemi wanawaagiza wataalamu kwanza kwa ajili ya kuona eneo na hali halisi.

“Nimemueleza Katibu Mkuu aweze kutenga fedha pamoja na kwamba wadau watatuchangia na sisi ambao tunawajibu wa kusimamia Afya ya msingi tutatoa fedha Shilingi Milioni 200 itatosheleza kabisa kuanza kujenga Majengo ambayo yatatosha kabisa kuanza huduma kama Kituo cha Afya,” amesema Mchengerwa.

Pia aliahidi kuwa atafika katika eneo hilo wa ajili ya kutembelea ili kuangalia utekelezaji wa mradi huo utakapoanza.

SOMA: Wapongeza ujenzi wa hospitali Karagwe

Hatua hiyo ilifikiwa katika mchakato wa utatuzi wa kero na changamoto za wananchi wa Mirerani katika sekta mbalimbali.

Habari Zifananazo

Back to top button