Sh tril.40 bajeti kugharamiwa na mapato ya ndani

DODOMA; BAJETI ya serikali ya mwaka wa fedha 2025/26 inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya shilingi trilioni 40.47.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwiguku Nchemba, wakati anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025.
“ Sura ya Bajeti inaonesha kuwa jumla ya shilingi 167 trilioni 56.49 zinatarajiwa kukusanywa na kutumika katika mwaka 2025/26.
“Bajeti hii inatarajiwa kugharamiwa na mapato ya ndani ya shilingi trilioni 40.47, misaada shilingi trilioni 1.07 na mikopo ya shilingi trilioni 14.95.
“ Kati ya mapato ya ndani yanayotarajiwa, mapato ya kodi ni shilingi trilioni 32.31, mapato yasiyo ya kodi shilingi trilioni 6.48, na mapato ya Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi trilioni 1.68.
“Aidha, mikopo inajumuisha shilingi trilioni 6.27 kutoka vyanzo vya ndani na shilingi trilioni 8.68 kutoka vyanzo vya nje,” amesema Waziri Nchemba.-