Shakila Mpomo atwaa fomu ubunge viti maalum

Shakila Mpomo amechukua na kurejesha rasmi fomu ya kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum kwa vijana Taifa kupitia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), akiwakilisha Mkoa wa Mtwara.
Shakila ni Mratibu Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la FB Empowerment linalojihusisha na utekelezaji wa afua mbalimbali za wanawake na vijana katika Mkoa wa Mtwara.