Shehena Bandari ya Dar es Salaam kufikia tani milioni 47.57

MAKUBALIANO yanayopendekezwa katika Azimio la serikali kuomba Bunge kuridhia mashirikiano kati ya Tanzania na Dubai yanalenga kuongeza shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 za mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33, sawa na ongezeko la asilimia 158.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliambia Bunge kuwa mbali na shehena, gharama ya usafirishaji wa mizigo kutoka nchi za nje kwenda nchi za Jirani, zitapungua kutoka dola za Marekani 12,000 mpaka kati ya dola 6,000 na 7,000 kwa kasha linalokwenda nchi ya Malawi, Zambia au DRC. “Hii italeta Watumiaji wengi kwenye Bandari ya Dar es Salaam,” amesema. ⤵️

Advertisement
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *