Sheria 9 kufanyiwa marekebisho

DODOMA; Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amewasilisha Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2025, huku sheria tisa zikitarajiwa kufanyiwa marekebisho.
Akiwasilisha muswada huo bungeni leo Juni 5, 2025, amezitaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa, Sura ya 200 na Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sura ya 177.
 
Amezitaja nyingine kuwa ni Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani, Sura ya 182; Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini, Sura ya 413; Sheria ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Sura ya 150 na Sheria ya Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, Sura ya 59.
 
Pia zipo Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Sura ya 268; Sheria ya Bandari, Sura ya 166; na Sheria ya Leseni za Usafirishaji, Sura ya 317.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button