Tumieni sheria kudhibiti udhalilishaji

ZANZIBAR : Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Kisiwani  Unguja Othman Ali Maulid amewataka wananchi wa Nungwi kuacha tabia ya kusuluhisha kesi za udhalilishaji katika ngazi za familia na badala yake wazifikishe katika vyombo vya sheria.

Akizungumza na wananchi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa utoaji wa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto, Maulid amewasisitiza wananchi kuendelea kutunza ushahidi ili kesi hizo za udhalilishaji wa kijinsia  ziweze kushughulikiwa kwa  utaratibu stahiki.

Nao baadhi ya wananchi wa Nungwi wameviomba vyombo vya sheria kuzidisha bidii katika kukabiliana na matukio ya udhalilishaji na kuyadhibiti  yasiendelea kutokea  ndani ya jamii.

SOMA : Vitendo vya ukatili mashuleni vidhibitiwe

 

Habari Zifananazo

Back to top button