Sheria ulinzi taarifa binafsi yakamilika

SERIKALI imekamilisha utungaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 iliyosainiwa Novemba, 2022 na kutangazwa katika Gazeti la Serikali Desemba 2, 2022 na imeanza kutumika rasmi Mei Mosi, mwaka huu.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia, Mathew Kundo ameyasema hayo leo Juni 20, 2023 bungeni mjini Dodoma akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Neema Lugangira (CCM).

Neema alitaka kujua, serikali ina mpango gani wa kuhuisha Sheria ya Makosa ya Mtandao na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi pamoja na Mkataba wa Malabo.

Alijibu swali hilo amesema, serikali imeweka mazingira wezeshi zaidi ya utekelezaji wa masuala yanayohusiana na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) nchini ikiwemo kufanikisha azma ya uchumi wa kidijiti.

Amesema sheria zinazofanyiwa mapitio kwa ajili ya kuhuishwa ni pamoja na sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015. Vile vile mikataba ambayo utaratibu umeanza kwa ajili ya kuridhiwa ni pamoja na Mkataba wa Malabo.

Habari Zifananazo

Back to top button