SHIRIKISHO la soka nchini Ureno limekanusha taarifa kuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo alitaka kuachana na timu hiyo na kurejea nyumbani, badaa ya kuwekwa benchi katika mchezo dhidi ya Uswis.
Awali zilienea taarifa kuwa Ronaldo alichukizwa na kitendo cha kuwekwa benchi na kuingia kipindi cha pili hali iliyoleta sintofahamu huku baadhi ya taarifa zikieleza kuwa Ronaldo angeweza kuachana na Ureno kwa kitendo hicho.
Taarifa hizo ziliambatanishwa na tetesi kuwa Ronaldo alishindwa kuelewana na kocha wake Fernando Santos na hata taarifa za kutaka kuachana na timu hiyo zilikuwa baina ya pande mbili.
Kwa upande wa kocha Santos amesema baada ya mchezo uliopita Ronaldo kuanzia nje, sasa anaweza kuanza katika michezo ijayo.