Sikinde kukiwasha leo usiku

BENDI ya Sikinde Ngoma ya Ukae, Baraza la Sanaa la Taifa kwa kushirikiana na Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa Alliance France leo Septemba 6 wanatumbuiza katika viwanja vya Alliance France jijini Dar es Salaam.

Akitoa taarifa hiyo Katibu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana amesema kwa mara nyingine tena wanakuletea tukio kabambe la burudani.

SOMA: Miaka 30 tangu afariki, Maneti bado ‘anaishi’

Advertisement

“Tulkio letu kabambe maarufu kama ‘Basata Social Club’ tukio hili mahususi linawakutanisha watu mbalimbali ikiwemo Viongozi, Watumishi wa Serikali na WanaDiplomasia kujumuika na kufurahi pamoja huku tukio hili.

Pia amesema kuwa tukio hilo linalenga kudumisha mahusiano na kubadilishana mawazo, kukumbuka muziki yetu ya wasanii kutoka Sikinde Mwana wa ukae.

SOMA: Small Jobiso kuja na bendi ya Singeli

“Haitakuwa kinyonge chini cha Bendi maarufu ya Muziki nchini Sikinde ngoma ya Ukae watahusika kutoa burudani, tukio hili litafanyika siku ya Ijumaa tarehe 06, Sept 2024 Leo karibu Las Vegas,” amesema.