Siku ya kuzaliwa: Miriam Odemba kuleta tabasamu wenye uhitajiTemeke

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO nguli nchini Miriam Odema amebariki na kufurahishwa na Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) kuwa mgeni rasmi katika sherehe za siku ya kuzaliwa.

Sherehe hizo zitakazofanyika Februari 19 katika Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu, Temeke, ambapo timu ya Taasisi ya Miriam Odemba Foundation itakuwa shuleni hapo kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji.

Tukio hili linatajwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha mshikamano kati ya wadau wa maendeleo na jamii kwa ujumla.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Miriam Odemba alieleza furaha na matumaini makubwa juu ya ushirikiano unaoendelea kukua kupitia Miriam Odemba Foundation, akisema:

“Nafurahi kuona kijana kama Kiliba kupokea ushirikiano wangu na Miriam Odemba Foundation. Kwa kweli nimefurahi sana kwani hii itafungua njia kubwa kwa watoto wa Jeshi la Wokovu kutamani kufika mbali. Pia hii ni chachu ya kuinua vipaji mbalimbali kwa watoto wa Jeshi la Wokovu, kuwatoa mamodel marais wa taifa la kesho”.

Kauli hiyo imepokelewa kwa hamasa kubwa, ikionesha dhamira ya dhati ya kuwekeza kwa watoto kama msingi wa maendeleo ya taifa la kesho.

Kupitia matukio kama haya, jamii inaendelea kushuhudia nguvu ya ushirikiano kati ya viongozi, taasisi na watu binafsi wenye moyo wa kujitolea.

Sherehe hizi hazitakuwa tu za kusherehekea siku ya kuzaliwa, bali zitakuwa jukwaa la matumaini, msukumo wa ndoto na uthibitisho kwamba kwa kushirikiana, Tanzania inaweza kuandaa viongozi, wabunifu na mabalozi wa kesho watakaoitangaza nchi.

Sherehe hizo zimepewa nguvu na GSM beverage, Mkombozi Digital Habari na Michuzi Blog.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button