Simba: Hongereni Yanga, tumejifunza

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewapongeza watani zao Yanga kwa kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika nakusema mafanikio hayo yamewapa somo.

Akizungumza na HabariLEO, kiongozi huyo amesema somo ambalo wamelipata kwenye mafanikio ya Yanga ni kusajili wachezaji bora wenye uwezo na uzoefu wa mashindano ya kimataifa na tayari wameuanza mchakato huo.

“Tumedhamiria kufanya usajili wa nguvu utakao kirudisha kikosi chetu kwenye ubora wa juu msimu ujao na hilo linawezekana kutokana na malengo tuliyokuwa nayo ya kuifanya Simba kuwa klabu kubwa Afrika,” amesema Try Again.

Yanga imetinga Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuifunga timu ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini mabao 2-1, na kufanya miamba hiyo ya Tanzania kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1 hiyo ni kutokana na ushindi wa mabao 2-0 iliyoupata kwenye mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback
4 months ago

[…] post Simba: Hongereni Yanga, tumejifunza first appeared on […]

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x