Simba kuikabili Ruvu Shooting leo

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba wanatarajiwa kushuka dimbani leo kuikabili Ruvu Shooting katika mchezo wa mzunguko wa 13 utakaochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Simba imetoka kuifunga Namungo katika mchezo uliopita bao 1-0 uliochezwa kwenye uwanja huo huo, huku Ruvu ikitoka kupoteza dhidi ya Azam FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Simba itakuwa ugenini katika mchezo huo ingawa ni uwanja wake wa nyumbani, lakini Ruvu Shooting mara nyingi inapocheza nao au Yanga hutumia uwanja huo ikiamini ni sehemu ya kuvuna mashabiki wengi wa timu hizo pendwa.

Katika michezo mitano iliyocheza Simba imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja, matokeo ambayo yaliwafanya kushuka kidogo hadi nafasi ya tatu kwa pointi 24 nyuma ya Azam FC na Yanga.

Wekundu hao walitoka kumkosa mchezaji wao muhimu, Cleatus Chama aliyekuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, lakini huenda akarejea katika mchezo huo.

Alikosa mechi dhidi ya Singida Big Stars, Ihefu na Namungo. Mchezo huo ni muhimu kwa Simba kushinda ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania taji la Ligi Kuu.

Mara ya mwisho kukutana na Ruvu Shooting msimu uliopita, Simba ilionekana vizuri ikishinda mechi mbili ya nyumbani na ugeni mabao 3-1 na 4-1. Inakutana na Ruvu Shooting ambao tangu kuanza kwa msimu huu wamekuwa wakipitia wakati mgumu kupata matokeo mazuri.

Katika michezo mitano iliyopita, Ruvu licha ya kuonekana kucheza vizuri imepata sare moja huku ikipoteza michezo minne. Timu hiyo imecheza jumla ya michezo 12, imeshinda mitatu, sare mbili na kupoteza saba ikiwa na pointi 11 hivyo, iwapo itapoteza leo pengine itaendelea kushuka nafasi ya chin.

Sasa iko iko katika nafasi ya 13. Inahitaji ushindi kujiondoa hatarini.

Kiufundi Simba bado iko vizuri katika safu ya ushambuliaji iliyofunga jumla ya mabao 20 na mchezaji hatari zaidi ni Moses Phiri anayeongoza kuifungia timu hiyo mabao sita na safu ya ulinzi imeruhusu mabao matano hivyo, bado kipa Aishi Manula na mabeki wake wanajua namna ya kulinda.

Ruvu imefunga mabao tisa ikionesha wazi namna inapata tabu kufunga lakini pia, ikiruhusu kuguswa mara 13 kwenye nyavu zake isipokuwa makini basi hata leo wanaweza kuchezea mvua ya mabao dhidi ya washambuliaji hatari wa Simba wenye uchu wa kufunga muda wote.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
trackback
18 days ago

[…] and Ruvu, Live Simba vs. Ruvu Shooting, Live Simba SC vs. Ruvu Shooting FC leo, Mabao yaliyofungwa Simba vs. Ruvu Shooting, Magoli Simba vs. Ruvu Shooting, and results Simba vs. Ruvu Shooting […]

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x