KLABU ya Simba Queens leo itaikabili PVP Buyenzi ya Burundi katika mchezo wa mwisho makundi katika michuano ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika(CAF) wanawake ukanda CECAFA.
Mchezo huo wa kundi B utafanyika kwenye uwanja wa Abebe Bekila uliopo mji mkuu Ethiopia, Addis Ababa.
SOMA: Simba Queens yatinga nusu fainali kufuzu CAF
Katika michezo miwili iliyotangulia Simba Queens imeifunga FAD Djibouti mabao 5-0 kisha kuichapa Kawempe Muslim ya Uganda mabao 3-0.
Mchezo mwingine wa kundi B ni kati ya Kawempe Muslim Ladies na FAD unaoendelea sasa.