Simba Queens yatinga nusu fainali kufuzu CAF

Moja ya hekaheka wakati wa mchezo kati ya Simba Queens na Kawempe Muslim.

MIAMBA ya soka la wanawake klabu ya Simba Queens leo imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika(CAF) Ukanda wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Mashariki na Kusini mwa Afrika(CECAFA) 2024 inayoendelea Ethiopia baada ya kuichapa Kawempe Muslim Ladies ya Uganda kwa mabao 3-0.

Mchezo huo umefanyika kwenye uwanja wa Abebe Bikila uliopo mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Advertisement

SOMA: Simba Queens wapania kumaliza kwa kishindo

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya FAD Djibouti ya Djibouti Agosti 19 Simba Queens ilishinda kwa mabao 5-0.

Simba Queens imekuwa ya pili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya CBE ya Ethiopia.