Dunia inasimama, Afrika inasimama, Afrika inatizama, matarajio ni makubwa, Simba wa Atlas ni wakubwa, wanashindana na wakubwa, zimebaki saa sita, mioyo ya wapenda soka inatikisika, leo Morocco watafanya nini mbele ya mabingwa wa Ulaya mwaka 2016, timu ya Taifa ya Ureno.
Wakati Simba wa Atlas iliyoweka historia kuingia hatua hiyo ikijiandaa kuchuana na timu hiyo, katika robo fainali ya Kombe la Dunia, matarajio ni makubwa kwa upande wao.
Walifika katika hatua hiyo kwa kuwaondosha ‘The Red Fury’ kwa mikwaju ya penalty.
Huku wakibeba matumaini ya Afrika, Morocco sasa wana matumaini ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kuvuka hadi nusu na endapo itafanya hivyo itakuwa ya kwanza kufanya hivyo kwa maana hakuna timu yoyote imewahi kufika hatua hiyo.Wakiwa wamefika robo fainali ya kwanza, mabingwa hao wa Afrika wa 1976 wanaonekana kukaribia kuvuka mafanikio ya Cameroon mwaka wa 1990, Senegal mwaka wa 2002, na Ghana mwaka wa 2010.
Kikosi hicho ambacho kinaonekana kimejipanga vyema, hakijapoteza mchezo wowote wa michuano hiyo tangu waliopoanza kampeni hizo kwenye hatua ya makundi na wamefungwa bao moja tu katika michezo yote.
“Jinsi walivyojijenga hadi kufikia hatua hii imekuwa jambo la kuvutia zaidi,” Michael Oti Adjei wa Media General Group wa Ghana, alisema “Walimfukuza kocha kabla ya mashindano na wakamleta mtu ambaye hakuogopa kufanya maamuzi na nidhamu ya kimbinu.