Klabu ya Simba imethibitisha kumnasa Sadio Ntibanzokinza na rasmi sasa atakuwa mchezaji wa klabu hiyo baada ya kutangazwa leo.
Simba imemtangaza kiungo huyo kupitia ukurasa wao wa Instagram. Simba SC imemsajili Saidi Ntibazonkiza kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea Geita Gold FC. Ntibanzokiza yupo jijini Mwanza kuungana na kikosi cha Simba kinachojiandaa na mchezo dhidi ya KMC.
Nyota huyo raia wa Burundi, aliwahi kuichezea Yanga na kuondoka kwenda Geita, uwezo wa kufunga, kutoa pasi za mabao umefanya Simba kuvutiwa na huduma yake.
Huo ni usajili wa kwanza kwa Simba katika dirisha dogo la usajili.
Comments are closed.