‘Sitapeliki’ kunusuru wateja mitandaoni

ARUSHA: KAMPENI ya kushughulikia masuala ya utapeli mtandaoni iitwayo “SITAPELIKI” imezinduliwa rasmi ikiwa mkakati wa serikali pamoja na watoa huduma za simu na intaneti kunusuru wateja.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo Februari 20, 2025 na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa sekta ya mawasiliano na teknolojia ya habari.

Amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa kuhusu mbinu zinazotumiwa na matapeli wa mtandaoni na kuwapa wananchi maarifa zaidi ya jinsi ya kujikinga dhidi ya majaribio mbalimbali ya ulaghai na hatimaye kujiepusha na udanganyifu unaofanywa na watu wachache wenye lengo la kujinufaisha.

Advertisement

Soma zaidi: Ikulu yaonya utapeli mtandaoni

Ametaja nukuu za ujumbe huo zitakazotolewa kuwa ni linda taarifa zako kwa kutumia nywila thabiti na tofauti kwa kila akaunti”, yenye mchanganyiko wa maneno, namba, alama na herufi kubwa na ndog ,“Usifuate maelekezo na kutoa nywila (neno siri) au namba yako yauthibitisho (OTP) kwa mtu yeyote.”

Tatu ni linda taarifa zako kwa kuepuka kubofya viunganishi (links) usivyovifahamu,Tunahimiza kuhakiki namba zako za simu kupitia *106#. Bofya *106# kisha chagua kuona namba zilizo sajiliwa na kitambulisho chako cha NIDA.

Amesisitiza iwapo utakuta namba usizo zifahamu tafadhali fika kwenye duka la mtoa huduma wako ili kupata ufafanuzi zaidi huku wanaokumbana na utapeli kuwasiliana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili matapeli hao washughulikiwe.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *