Song atundika daluga
KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Alexander Song amestaafu kucheza soka.
–
Song ,36, raia wa Cameroon alianza kucheza soka akiwa Bastia ya Ufaransa, kabla ya 2006 kwenda Arsenal kwa mkopo na baadaye kusajiliwa moja kwa moja.
–
Mwaka 2012 alijiunga na Barcelona, baada ya misimu miwili, Song alirejea England kunako West Ham United, baada ya msimu mmoja alijiunga na Rubin Kazan ya Urusi.
–
Mpaka anastaafu, Song alikuwa akikipiga AS Arta/Solar7 ya nchini Djibouti.