Spika: Bunge likivunjwa serikali inaendelea na kazi

SPIKA wa Bunge, Dk Tulia Ackson amesema bunge likivunjwa haina maana serikali itakuwa likizo bali itaendelea na kazi yake.

Alitoa kauli hiyo bungeni Dodoma jana baada ya baadhi ya wabunge kuonesha wasiwasi katika kuuliza maswali kana kwamba hayawezi kufanyiwa kazi sababu ni bunge la mwisho.

“Bunge likivunjwa kwa muda serikali haiendi likizo,” alisema.

Dk Tulia alisema ni wajibu wa wabunge kuendelea kuuliza maswali kwa serikali kwa sababu hoja za wabunge zinaendelea kuchukuliwa na serikali.

“Ndiyo maana bunge lilitunga sheria ya kuunda Tume ya Mipango ambayo ipo kazini na inatekeleza wajibu wake na inachukua hoja zinazohusu serikali na kuzifikisha kwa taasisi husika,” alisema.

Wabunge wanapouliza maswali, hoja au kutoa michango katika hoja ya serikali hawafanyi kwa ajili yao bali kwa ajili ya wananchi kutoka katika maeneo yao.

“Serikali inaendelea, bunge linavunjwa kwa muda, mbunge anapoleta hoja si yeye binafsi kwa niaba ya uhitaji wa wananchi, halijalishi ni la wakati gani,” alisema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button