‘Stay humble’ Emirates pamoto

ENGLAND: Manchester City VS Arsenal: Septemba Uwanja wa Etihad
Arsenal waliongoza, kisha Leandro Trossard akala umeme wakawa 10
Arsenal ikazidiwa City wakaanza kushambulia mfululizo, Arteta hakuwa na jinsi zaidi ya kupaki basi dakika za jioni John Stones akasawazisha na ubao kusomeka 2-2.
Wakati wakishangilia, Erling Haaland alirusha mpira kwenye kichwa cha beki wa Arsenal, Gabriel alilalamika lakini malalamiko yake hayakuwa na faida.
Filimbi ya mwisho ilipopulizwa kuashiria kumalizika kwa mchezo, Haaland alimwambia meneja wa Arsenal Mikel Arteta ‘Stay Humble’ Kaa Kwa Unyenyekevu wakati wakipeana mikono kuagana. Alipohojiwa Gebriel alisema: “Tunawasubiri Emirates”.
Tangu hapo ‘Stay Humble imekuwa maarufu sana, leo wanakutana tena saa 1:30 usiku uwanja wa Emirates nani atakaa kwa unyenyekevu?



