STEM kuchagiza ushiriki, maendeleo ya kijamii, kiuchumi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amesema Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi yanalenga kuhamasisha na kuongeza ushiriki wa wanawake na wasichana katika nyanja za Sayansi, Uhandisi na Hisabati (STEM).
Prof. Mushi amesema hayo leo Februari 11 jijini Dodoma, ambapo ameongeza kuwa Tanzania tangu mwaka 2021 imeungana na nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha ili kuchagiza ushiriki na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *