Sudan: Kambi ya wakimbizi Zamzam yashambuliwa

SUDAN : MASHIRIKA ya Kimataifa ya misaada yameelezea kukerwa na shambulio lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la RSF katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini Sudan, ambapo watu wasiopungua 112 walipoteza maisha, ikiwa ni pamoja na watoto zaidi ya 20.

Shambulio hilo, lililotokea katika eneo la Darfur, lilihusisha uharibifu wa jiko la kijamii la kambi hiyo, na kuchochea hofu miongoni mwa wakimbizi 500,000 wanaoishi katika eneo hilo.

Makadirio yanatoa taswira mbaya zaidi, yakionyesha kuwa idadi ya wakimbizi inakaribia milioni moja. Kambi ya Zamzam inaelezwa kuwa inakabiliwa na changamoto kubwa huku mji wa Al Fashar, ulio karibu, ukishikiliwa na kundi la RSF kwa karibu mwaka mzima.

Advertisement

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema watoto zaidi ya 140 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni katika eneo hilo.

SOMA: Jeshi la Sudan larejesha udhibiti wa Ikulu

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *