Wachimbaji 11 wa dhahabu wapoteza maisha

KHARTOUM,SUDAN : KAMPUNI ya Rasilimali ya Madini Sudan (SMRC) imethibitisha kuwa wachimbaji 11 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kuangukiwa na mgodi katika eneo la Kirsh al-Fil, jangwa la Howeid, kati ya miji ya Atbara na Haiya linalodhibitiwa na jeshi.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, wachimbaji wengine saba walinusurika lakini walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu. Hata hivyo, haijafahamika ni lini ajali hiyo ilitokea.

SMRC ilieleza kuwa mgodi huo ulikuwa umesitishwa awali kutokana na hofu ya usalama wa wachimbaji, lakini haikubainisha ni kwa vipi shughuli ziliendelea hadi tukio hilo kutokea. SOMA: Kampuni yaaminiwa upimaji madini

Pamoja na kuwa Sudan ni mmoja wa wauzaji wakubwa wa dhahabu Barani Afrika, ajali za migodi zimekuwa zikijirudia mara kwa mara kutokana na viwango duni vya usalama kwenye maeneo ya uchimbaji, hasa yale ya wazi na yasiyosimamiwa kikamilifu na serikali.

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button